Alichosema Wolper kuhusu ishu ya Nicole 

Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza mwingizaji na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amezungumza kuhusu  kesi inayomkabili mwigizaji mwenzie Joice Mbaga ‘Nicole’. Ambaye alifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi kwa kupokea amana (fedha) kutoka kwa umma bila kibali cha Benki Kuu (BoT).

Wolper ameweka wazi kuwa hajawahi kusikia skendo yoyote ya msanii huyo kuwa mwizi, huku akidai Sh 180 milioni kwa Nicole ni pesa ndogo.

“Sh 180 milioni ni hela ndogo sana na kwa msanii kama Nicole ninavyomjua mimi. Sidhani kama fedha ndogo kama ile inaweza kumchafua, unajua sisi binadamu kuna vitu vingi sana lakini pia tunapitia vitu vingi sana. 

“Kwa hilo naweza kusema. Sidhani kama ni hela ambayo inaweza kumshinda Nicole kwa sababu kama yeye ni mpambanaji, nadhani mnamuona anavyopambana kila siku. Anavyopiga domo, anatangaza hadi matangazo ambayo hayafai kwa hiyo ni mtafutaji ni mpambanaji,”amesema Wolper

Ikumbukwe Nicole alikaa rumande kwa siku 15 na mwenzake Rehema Mahanyu (31), wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, waliachiwa Machi 17, 2025, kwa dhamana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *