
Ufaransa itajibu “mara moja,” “kwa uthabiti, na kwa uwiano” kwa uamuzi “usioeleweka” wa Algeria wa kuwafukuza maafisa wengine wa Ufaransa katika ardhi ya Algeria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot amesema siku ya Jumatatu, Mei 12, 2025. “Huu ni uamuzi usioeleweka na wa kikatili,” mkuu wa diplomasia ya Ufaransa amejibu wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Siku moja kabla, Algiers iliripoti kufukuzwa kwa maafisa wapya wa Ufaransa nchini Algeria kwa afisa wa ubalozi wa Ufaransa nchini Algeria.
Wanadiplomasia wa Ufaransa nchini Algeria imiongoni mwa Wafaransa wengine waliochukuliwa na hatua ya kufukuzwa nchini Algeria na mamlaka ya nchi hiyo. Mamlaka ya Ufaransa imethibitisha kwamba maafisa waliotumwa kwa muda mjini Algiers wametakiwa kufunga virago vyao na kuondoka nchini. Hawaelezi idadi, lakini Algeria inazungumza kuhusu maafisa kumi na tano.
Alipoitwa Mei 11, 2025 na mamlaka ya Algeria,afisa huyo wa ubalozi wa Ufaransa mjini Algiers aliarifiwa kuhusu kufukuzwa kwa maafisa ambao kwa sasa wako kwenye misheni ya muda ya usaidizi nchini humo.
Algeria inadai kwamba walitumwa kinyume na sheria na kwa hivyo wanapaswa kurejeshwa nyumbani mara moja. Katika ujumbe uliochapishwa siku ya Jumapili jioni, APS, shirika la habari la serikali ya Algeria, limetaja “maafisa wasiopungua kumi na tano ambao walitarajia kushikilia nyadhifa za kidiplomasia au kibalozi bila kutoa arifa rasmi au maombi ya kibali yanayofaa kama inavyotakiwa na taratibu zinazotumika.”
“Uamuzi huu sio kwa maslahi ya Algeria wala sio kwa maslahi ya Ufaransa”
Paris inathibitisha kufukuzwa kwa watu hao, lakini sio takwimu hii. Diplomasia ya Ufaransa inapingana na uhalali huo, na inaamini kwamba watu hawa waliokuwa na pasipoti za kidiplomasia hawakuhitaji utaratibu wowote maalum wa misheni ya chini ya siku 90.
Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noël Barrot amejibu: “Kuondoka kwa maafisa kwenye misheni ya muda sio haki na hakuna uhalali. Na kama nilivyofanya mwezi uliopita, tutajibu mara moja, kwa uthabiti na kwa namna inayolingana na madhara kwa maslahi yetu. […] Huu ni uamuzi ambao ninachukia kwa sababu sio kwa maslahi ya Algeria wala kwa maslahi ya Ufaransa.”
Mamlaka ya Algeria pia imeripotiwa kuwa mchakato wa kuidhinishwa kwa mabalozi tisa nchini Ufaransa ulikuwa umezuiwa kwa miezi kadhaa.
Biashara mpya
Katikati ya mwezi wa Aprili, duru ya kwanza ya mapigano ilifanyika kwa kufukuzwa kwa maafisa kumi na wawili wa Ufaransa kutoka Algeria, kufuatia kukamatwa huko Ufaransa kwa maafisa wa kibalozi katika kesi ya utekaji nyara wa mshawishi mkosoaji wa mamlaka ya Algeria. Ufaransa ilijibu kwa kuwafukuza maafisa kumi na wawili wa ubalozi wa Algeria na kumuita tena balozi wake, ambaye bado yuko Paris leo.
Tangu wakati huo, uhusiano kati ya nchi hizo mbili “umesitishwa kabisa,” kulingana na maneno yaliyotumiwa na Jean-Noël Barrot katika mahojiano siku ya Jumapili. Ziara kadhaa za maafisa wa Ufaransa zimeahirishwa katika wiki za hivi karibuni.