Algeria yamwita balozi wa Ufaransa kulalamikia vitendo vya ‘kichokozi’ dhidi ya raia wake katika viwanja vya ndege vya Paris

Algeria imemwita balozi wa Ufaransa mjini Algiers, Stephane Romatet jana Jumanne, na kuwasilisha malalamiko makali ya kupinga “mwenendo wa kichochezi” wa maafisa wa Ufaransa dhidi ya raia wa Algeria katika viwanja vya ndege mjini Paris.