
Mamlaka za Algeria hapo jana zilitangaza kufunga anga yake kwa nchi ya Mali pamoja na kumrudisha nyumbani balozi Wake mjini Bamako, hatua inayokuja baada ya Mali kuituhumu Algiers kudungua ndege isiyo na rubani juma moja lililopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika kujibu hatua ya Algeria, utawala wa Bamako nao ulitangaza kufunga anga yake kwa ndege zote zinatoka au kuelekea Algeria.
Katika taarifa yake, wizara ya ulinzi ya Algeria imesema kuwa, kufuatia mfululizo wa ukiukaji wa makusudi wa matumizi ya anga yake na nchi ya Mali, Algiers imeamua kufunga anga lake kutumiwa na ndege zinazoingia au kutoka Bamako.
Algeria pia imemuita nyumbani balozi wake wa Niger, ikijibu hatua iliyochukuliwa na Niamey pamoja na Burkina Faso, ambazo ziliwarejesha nyumbani mabalozi wake.
Mataifa ya Niger, Mali na Burkina Faso yalitangaza kuwaondoa mabalozi wake nchini Algeria kuonesha uungaji mkono wao kwa utawala wa Bamako, ambao umeishutumu Algiers kufadhili makundi ya wanajihadi kutatiza usalama kwenye nchi zao.