
Mahakama nchini Algeria imemhukumu mwandishi maarufu wa vitabu, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria Boualem Sansal, ambaye amekuwa kizuizini tangu mwezi wa Novemba, kifungo cha miaka mitano jela sku ya Alhamisi, Machi 27, nusu ya hukumu iliyoombwa na upande wa mashtaka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Boualem Sansal, ambaye kesi yake ni kitovu cha mzozo wa mvuto usio na kifani na Ufaransa, ameshutumiwa haswa kwa kuhatarisha uadilifu wa eneo la Algeria kwa kuchukua, katika chombo cha habari cha Ufaransa cha mrengo wa kulia, msimamo wa Morocco kulingana na madai ambayo eneo lake lilikuwa limekatwa kwa faida ya Algeria chini ya ukoloni wa Ufaransa.
Mahakama ya jinai ya Dar El Beida, karibu na Algiers, imetangaza, “mbele ya mshtakiwa, kifungo cha miaka mitano jela,” pamoja na faini ya dinari 500,000 za Algeria (karibu euro 3,500), kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.
Wakati wa kesi yake mnamo Machi 20, mwendesha mashtaka aliomba kifungo cha miaka kumi jela kwa mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 80.
Suala la kidiplomasia kati ya Algiers na Paris
Kabla ya uamuzi huu wa mahakama, wachambuzi kadhaa waliamini kwamba kupunguzwa kwa hukumu au kuhukumiwa kufuatiwa na msamaha wa rais kunaweza kupunguza mvutano kati ya Paris na Algiers. Mgogoro ulioelezewa kuwa “mzito zaidi katika miongo kadhaa”.
Kukamatwa kwa Boualem Sansal Novemba mwaka jana huko Algiers kulizidisha mvutano mkubwa kati ya nchi hizo mbili. Mvutano huu ulichochewa tena na tangazo la Emmanuel Macron kwamba anaunga mkono mpango wa Morocco wa kujitawala chini ya mamlaka ya Morocco kwa Sahara Magharibi, eneo linalozozaniwa.
Wakili wake Mfaransa, François Zimeray, ametoa wito kwa Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune kuonyesha “ubinadamu” katika suala hili. “Umri wake na hali ya afya yake hufanya kila siku ya kifungo kuwa ya kikatili zaidi. “Natoa wito kwa rais wa Algeria: haki imeshindwa, angalau basi ubinadamu utawale,” ameandika Bw. Zimeray kwenye mtandaowa kijamii wa X, katika dokezo la msamaha unaowezekana wa mkuu wa nchi.