
Nchini Algeria, jaji wa mahakama ya jinai ambaye Boualem Sansal alifikishwa mbele yake anatazamiwa kutoa uamuzi wake leo Alhamisi, Machi 27. Mwandishi huyo raia wa Algeria, aliyekamatwa katikati ya mwezi Novemba, anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka kumi jela kwa maoni yake aliyoyatoa katika chombo cha habari cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa. Hukumu hii imesababisha mzozo ndani ya wanasiasa wa Ufaransa, ambao wameanzisha uhamasishaji wa kutaka kuachiliwa kwake.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Boualem Sansal alikamatwa muda mfupi baada ya kushuka kwenye ndege kwenye uwanja wa ndege wa Algiers mnamo Novemba 16. Haraka sana, alishutumiwa na mamlaka ya Algeria kwa hatarisha uadilifu wa eneo la nchi hiyo na kwa ujasusi na kambi za kigeni kwa maoni aliyoyatoa juu ya suala tete la mpaka kati ya Morocco na Algeria.
Wiki iliyopita, wakati wa kesi iliyochukua takriban dakika 30, Boualem Sansal aliweza kujitetea, licha ya kuwepo kwa wakili aliyepewa jukumu lake. Mwanasheria wake Mfaransa, François Zimeray, hakuwahi kupata visa ya kusafiri kwenda Algiers.
Ingawa mashtaka ya upelelezi na adui yalitupiliwa mbali, upande wa mashtaka bado uliomba kifungo cha miaka kumi jela na faini ya dinari milioni 1 (takriban euro 298,000) dhidi ya mwandishi huyo mwenye umri wa miaka 80 ambaye anaugua saratani. Anashutumiwa haswa kwa kuhatarisha uadilifu wa eneo la kitaifa, kuhatarisha usalama wa taasisi na jeshi na kuhatarisha usalama wa taifa.
Kesi inayomkabili raia mwenzetu ni kesi ya mtu huru ambaye anakataa kurejesha macho nyuma kuhusu ukweli au kuinamisha macho yake mbele ya vitisho vikali na vya kikatili. Pia ni kesi inayojikita kwa demokrasia na kwa haki za binadamu, anasema Arnaud Benedetti, amwanzilishi wa kamati ya usaidizi ya mwandishi wa huyo raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria, ambaye analani kesi aliyoiita ya kisiasa.
Jambo hili limezua taharuki miongoni mwa wadau wa kisiasa nchini Ufaransa. Mnamo Januari 27, pendekezo la azimio la Ulaya liliwasilishwa na wanachama wa chama cha Renaissance wanaotaka kuachiliwa kwake. Azimio ambalo liliwekwa kwenye ajenda ya Bunge la Kitaifa mnamo Jumatano, Aprili 30.