Al-Azhar: Gaza itabaki kuwa Palestina na ardhi ya Kiarabu; UN, EU pia zapinga mpango wa Trump

Taasisi ya Al-Azhar ya Misri, imelaani mpango wa Rais wa Marekani wa kuwatimua Wapalestina kwa nguvu katika eneo la Ukanda wa Gaza, ikisisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza ni ardhi ya Wapalestina na Waarabu na itabaki hivyo daima.