Hatimaye Al Hilal ya Sudan wamepangwa na kingingi Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi za kwanza zikipigwa Aprili Mosi.
Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo ndiyo timu yenye mafanikio zaidi kwenye michuano hiyo barani Afrika, ikiwa inapewa nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali.
Al Hilal chini ya Kocha mzoefu, Florent Ibenge ambayo ilikuwa kundi moja na Yanga kwenye michuano hii itatakiwa kuhakikisha inafanya kazi kubwa ili kuwazima Waarabu hao ambao wameshatwaa ubingwa huo mara 12. Huku Hilal ikiwa haina mafanikio makubwa huku.

Hata hivyo, mechi nyingine kali ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa ni kati ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusinia ambao watavaana na Esperance de Tunis, zikiwa ni timu ambazo ambazo zinarekodi kubwa pia kwenye michuano hii.
Mamelodi ambayo msimu uliopita iliishia hatua ya nusu fainali ikitolewa na Tunis, kumbukumbu yake kubwa zaidi kwenye michuano hiyo ni kutwaa ubingwa mwaka 2006, itatakiwa kufanya kazi kubwa wakati watakapokutana na Waarabu hao ambao wameshatwaa ubingwa huo mara nne, huku mara ya mwisho ikiwa mwaka 2019.
Mechi nyingine kali ni MC Algier ambao hawana rekodi nzuri kwenye michuano hii watacheza na wababe wa Afrika Kusini Orlando Pirates ambao walipotea kwa muda na sasa wamarejea wakiwa hawana rekodi nzuri nao baada ya kufika fainali mwaka 2013. Pyramids ya Misri itavaana na Waarabu wenzao AS FAR ya Morocco ambayo inachipukia kwa kasi kubwa kwenye soka la Afrika.