Utawala wa Kremlin unasema agizo la rais Vladimir Putin kwa wanajeshi wake kutoshambulia miundombinu ya nishati nchini Ukraine bado linatumika licha ya kuituhumu Kyiv kwa kwenda kinyume mara kadhaa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kituo cha nishati nchini Urusi karibu na eneo la mpaka na Ukraine ambacho kilikuwa kinasafirisha gesi kwenda barani Ulaya kilishambuliwa usiku, shambulio ambalo Moscow na Kyiv zinatuhumiana kwa kuhusika.
“Kila mtu anaweza kuona namna tunaweza kuliamini neno kutoka kwa Zelensky pamoja na wawakilishi wengine wa utawala wa Kyiv,” amesema msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov katika mkutano na waandishi wa habari.
Putin aliagiza usitishaji wa mashambulio wenye marsharti wa siku 30 dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine Jumanne ya wiki hii baada ya mazungumzo ya njia ya simu na mwenzake wa Marekani Donald Trump.

Alhamis ya wiki hii, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema kwamba Moscow ilikuwa inaendelea kushambulia miundombinu ya nishati na hakuna kilichobadilika licha ya matamshi ya rais Putin.
Wajumbe kutoka pande zote kwenye mzozo wa Ukraine wanatarajiwa kukutana na maofisa wa Marekani nchini Saudi Arabia siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.
Rais Trump amesisitiza kwamba anaweza kuumaliza mzozo huo wa miaka mitatu sasa.