
Viongozi wa nchi na serikali, wamekutana jijini Addis Ababa kujadili kuundwa kwa taasisi ya Afrika itakayoshughulikia utathmini wa mikopo kwa nchi ya Afrika hii ikiwa ni mkakati wa Afrika kuondoka kwenye mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia utathmini wa mataifa ya Afrika kabla kupewa mikopo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Viongozi waliohudhuria kikao hicho wameendelea kulalamikia kuendelea kubaguliwa nchi za Afrika inapokuja mikopo.
Wamesema kuwa nchi za Afrika zinalazimika kutimiza masharti makali kabla kupewa mikopo ikiwemo kushinikizwa kuwa na sere za kiuchumi zinazokandamiza au kupewa riba ya juu.
Akizungumza katika kikao hicho rais wa Kenya, pia mwenyekiti wa jumuiya ya Afrika Mashariki, William Ruto amesema, kwa muda Afrika imetathminiwa kwa vigezo ambavyo haviendani na hali halisi.
” Mashirika ya kimataifa ya kutathmini uwezo wa kukopa,yametuangusha,wanategemea vigezo visivyo,na mfumo wote ni wa kibaguzi,matokeo yake ni wanatoa picha isiyotenda haki kwa uchumi wetu na inaleta madhara kwa sababu inaelezea hali potovu kuhusu uwezo wa kupata mikopo kama nchi na bara haya yote yakichangia gharama ya kupata mikopo kuwa kubwa,” amesema Rais Ruto.
Naibu mwenyekiti wa tume ya AU Monique Nsanzabagnwa ambaye pia anasimamia utawala na fedha, amesema hatua ya kuundwa kwa taasisi hiyo ni ukombozi wa kifedha kwa Afrika.
“Afrika inainuka, na ni wakati wetu kudai nafasi yetu kiuchumi,kuundwa kwa taasisi hii ya kutatmini uwezo wa kupata mikopo ni hatua ya kijasiri inayohitajika ili kuelekea Afrika kupata utambulisho ambao hautegemei mashirika ya nje,ila inafahamika kuhusiana na hali yake halisi.” Ameeleza Naibu mwenyekiti wa tume ya AU Monique Nsanzabagnwa
Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa linalokadiria hali ya chumi za Afrika ,The Africa Peer Review bara la Afrika limepoteza nafasi za ufadhili zenye thamani ya dola bilioni 55 kutokana na ubaguzi huu wa kifedha.
Carol Korir- Addis Ababa.