Afrika Kusini: Ziara ya kihistoria ya rais wa Ukraine yakatizwa na vita

Rais wa Ukaine Volodymyr Zelensky alikuwa Afrika Kusini siku ya Alhamisi Aprili 24. Alipokelewa na Rais Cyril Ramaphosa katika ikulu ya rais mjini Pretoria. Ziara fupi kuliko ilivyopangwa, kwani Kyiv ililengwa na mashambulio makali na mabaya sana ya Urusi. Moja ya shambulio muhimu zaidi katika mji mkuu wa Ukraine tangu kuanza kwa vita.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu maalum mjini Pretoria, Valentin Hugues

Kabla ya kupanda ndege kurudi Kyiv, Volodymyr Zelensky alizungumza na vyombo vya habari. Alikumbusha umuhimu wa nafasi ya Afrika Kusini, na bara zima kwa ujumla, katika kufikia amani nchini mwake.

Mkutano wa kihistoria ulifanyika Aprili 24 nchini Afrika Kusini, katika hafla ya ziara rasmi ya kwanza ya rais wa Ukraine katika nchi ya Kiafrika, ikionyesha nia ya kukaribia bara hilo.

“Putin hathamini uwepo wa Ukraine barani Afrika. Urusi inataka uwepo wa kipekee. Lakini tuna imani kuwa rais wa Afrika Kusini na washirika wengine barani Afrika watasaidia kumlazimisha Putin kuunga mkono usitishaji vita kamili na bila masharti na kumaliza vita.”

Afrika Kusini inathibitisha jukumu lake kama mpatanishi

Na kama nchi isiyofungamana na upande wowote, Afrika Kusini imethibitisha nia yake ya kuwa nchi ya upatanishi. Wiki hii tu, kabla tu ya ziara ya Zelensky, Cyril Ramaphosa pia alizungumza kwa simu, na Vladimir Putin, na kisha na Donald Trump.

“Uzoefu wetu wenyewe wa safari kutoka kwa jinamizi la ubaguzi wa rangi hadi demokrasia unatufundisha umuhimu wa kushirikisha pande zote kwenye mgogoro ili kufikia amani. Ikiwa kuna jambo moja ambalo historia yetu imetufundisha, ni kwamba diplomasia na mazungumzo yana nguvu zaidi kuliko silaha yoyote.”

Volodymyr Zelensky alilazimika kukatisha ziara yake huko Pretoria ili kurejea kwa haraka Kyiv, kufuatia moja ya mashambulio makubwa ya Urusi kwenye mji mkuu wa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *