Afrika Kusini yapinga ‘diplomasia ya kipaza sauti’ na ya kibabe ya Trump

Huku Rais wa Marekani, Donald Trump, akiendelea kuingilia masuala ya ndani ya Afrika Kusini, serikali ya Pretoria imetangaza kwamba haitajihusisha na diplomasia isiyojenga ya “ya kipaza sauti” na ya bwabwaja ya Marekani.