Afrika Kusini yaipongeza ICC kwa kutoa waranti wa kukamatwa Netanyahu na Gallant

Serikali ya Afrika Kusini imepongeza hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya kutoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu,pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Idara ya uhusiano wa kimataifa wa Afrika Kusini (Dirco) imesema kutolewa kwa hati ya kuwakamata viongozi hao ni jambo la busara kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu huko Gaza.frika Kusini imesisitiza kuendelea kujitolea kwake kuheshimu sheria za kimatifa na kutaka mataifa ambayo ni wanachama kutekeleza majukumu yao kulingana na utaratibu uliowekwa na sheria za Roma.

Jana Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant, wakituhumiwa kutenda jinai za vita.

Mwezi Mei mwaka huu, Karim Khan, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), alitaka itolewe hati ya kumkamata waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, na waziri wake wa vita Yoav Gallant kwa sababu ya kutenda jinai katika vita vya utawala huo dhidi ya watu wa Ukanda wa Ghaza huko Palestina.