
Afrika Kusini imeanza kuimarisha uwepo wake wa kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Takriban siku kumi zilizopita, Pretoria ilituma vifaa vya kijeshi na wanajeshi, kati ya 400 na 8,000 kulingana na vyanzo, katika jiji la Lubumbashi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Afrika Kusini ilipoteza wanajeshi wake 14 katika vita vya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya kidemkorasia ya Congo kati ya jeshi la FARDC na washirika wake pamoja na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waliofaulu kuingia katika mji wa Goma.
Taarifa zinasema Afrika Kusini sasa imeongeza wanajeshi wengine ndani ya kikosi cha kulinda amani Monusco pamoja na SamiDRC kikosi cha SADC.
Wanajeshi hao wanakadiriwa kuwa kati ya 700 na 800 waliotumwa Lubumbashi juma lililopita, ambapo mjadala umeibuka nchini Afrika Kusini tangu kutokea kwa vifo vya wanajeshi 14 waliouawa huko Goma na kikosi hiki kipya kinatumwa huko bila hata hivyo bunge kufahamishwa.
Msemaji wa jeshila FARDC Jenerali Sylvin Ekenge amekataa kuthibitisha au kukanusha taarifa hiyo lakini duru za kiusalama mjini Lubumbashi zimethibitisha kutumwa kwa wanajeshi 400, ambapo kabla ya hapo ndege za kijeshi za Afrika Kusini ziliwasilisha vifaa vya kijeshi na wanajeshi kadhaa.
Lakini swala lililopo ni je kwa nini Lubumbashi kwenye umbali wa kilomita 1700 na uwanja wa mapambano, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, je wataelekea kwenye uwanja wa mapambano?