Afrika Kusini: Uhusiano wetu na Iran na kuipandisha kizimbani Israel ndiyo sababu ya hasira za Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imeashiria hatua ya rais wa Marekani, ya kufanya propaganda kubwa dhidi ya nchi hiyo kutokana na uhusiano mzuri wa Afrika Kusini na Iran na hatua ya Pretoria ya kufungua kesi ya kuadhibiwa viongozi watenda jinai wa Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ na kusema kuwa, inasikitisha kuona Marekani inaendesha propaganda chafu dhidi ya Afrika Kusini.