Afrika Kusini: Kumng’oa pembe faru husaidia kiasi kikubwa kupunguza ujangili, utafiti wagundua

Kulingana na utafiti uliofanywa kati ya mwaka 2017 na 2023 katika Mbuga ya Kitaifa ya Kruger maarufu Afrika Kusini, iliyochapishwa Juni 5 kwenye jarida la Science, kuwang’oa faru pembe kumefanya kupungua kwa karibu 80% ya ujangili. Afrika Kusini, ambayo ni nchi inayoongoza kwa idadi kubwa zaidi ya vifaru duniani, ikiwa ni pamoja na faru mweusi aliye hatarini kutoweka, imeathiriwa pakubwa na uwindaji haramu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Afrika Kusini, takriban faru 34 huuawa kila mwezi, kulingana na Waziri wa Mazingira wa Afrika Kusini, katika nchi hii ambayo bado ilikuwa na faru 16,000 mwishoni mwa mwaka 2023. Lakini dola milioni 74 zilizotumika kati ya mwaka 2017 na 2023 kulinda aina hii, wala kupelekwa kwa walinzi wa mazingira na mbwa havikuzuia tabia hii ya uwindaji haramu. Hatua hizi, hata hivyo, zilipelekea kukamatwa kwa wawindaji haramu wapatao 700.

Katika kipindi hiki, karibu faru 2,000 waliwindwa kwa ajili ya pembe zao, ambao walichukuliwa kimakosa kuwa aphrodisiac katika nchi nyingi za Asia. Pia ni ishara ya ufahari wa kijamii. “Ukosefu wa usawa wa kijamii na kiuchumi unahimiza idadi kubwa ya watu walio hatarini na waliohamasishwa kujiunga na mashirika ya uhalifu au kuwawinda, hata wakati hatari ni kubwa,” watafiti wanasisitiza. Rushwa ina jukumu katika jambo hili, kwani magenge yanadokezwa na watoa habari, na kuwaruhusu kukwepa kukamatwa.

Kwa upande mwingine, kukatwa pembe kwa zaidi ya faru 2,000 kumefanya kupungua kwa asilimia 78 kwa ujangili. Utafiti huo katika jarida la Science unaangazia kwamba “athari za kukata pembe kwenye biolojia ya vifaru bado haziko wazi, lakini kwamba mazoezi hayana athari kwa maisha na uzazi wao.”

Soma piaAfrika Kusini: Ujangili wa faru waanza tena baada ya kupungua kutokana na Corona

Hata hivyo, watafiti wanasema, kuondolewa kwa pembe mara kwa mara ni muhimu. Umaskini unasukuma watu wengi walio katika mazingira magumu kujiunga na mashirika ya uhalifu kufanya ujangili. Kwa mfano, faru wasio na pembe wameuawa na wawindaji haramu wakilenga mashina yao na kuota upya kwa pembe. Katika soko la biashara haramu, bei ya pembe za faru inakaribiana na ile ya dhahabu na kokeini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *