
Wanajeshi wa Afrika Kusini wawalioondoka hivi karibuni Mashariki mwa DRC kutoka kikodi cha SADC wameanza kukusanyika nchini Tanzania na wengi wao wanatarajiwa kurejea nyumbani mwezi huu, mkuu wa majeshi amesema Jumapili.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Kama sehemu ya kuondoka hatua kwa hatua mashariki mwa DRC, zoezi lililoanza Aprili 29, wanajeshi wanatakiwa kuondoka DRC kwa njia ya barabara kupitia Rwanda kabla ya kuingia Tanzania, Jenerali Rudzani Maphwanya amesema.
Kutoka Tanzania, watarejea Afrika Kusini kwa njia ya baharini na angani mwishoni mwa mwezi Mei, mesema.
Wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichotumwa mashariki mwa DRC Desemba 2023 wakati kundi la waasi la M23 likisonga mbele katika mashambulizi yake mashariki mwa DRC.
M23 sasa inadhibiti maeneo makubwa katika eneo hili lenye utajiri wa madini.
Malori 13 yaliyokuwa yamebeba wanajeshi 57 wa kikosi cha kulinda amani cha SADC (SAMIDRC) tayari yamekusanyika sehemu moja nchini Tanzania, Maphwanya amewaambia waandishi wa habari.
Kundi linalofuata linatarajiwa kuondoka wiki ijayo, amesema.
SADC iliamua kusitisha misheni yake ya SAMIDRC katikati ya mwezi Machi baada ya wanajeshi wake 17, wengi wao wakiwa Waafrika Kusini, kuuawa katika mashambulizi ya M23 mwezi Januari. Walikuwa wamekwama mjini Goma tangu wakati huo.
Kundi hilo lilithibitisha wiki iliyopita kuwa kuondoka huko kumeanza, lakini hawakutoa maelezo yoyote.
Mnamo Aprili 30, uhamishaji tofauti ulianza kwa mamia ya askari na maafisa wa polisi wa Kongo ambao walikuwa wamenaswa kwa miezi kadhaa katika kambi za Umoja wa Mataifa huko Goma baada ya mji wa mashariki mwa DRC kutekwa na waasi wa M23, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilisema.
– Msiache chochote nyuma –
Wakuu wa ulinzi wa SADC waliifahamisha M23 kwamba “wataondoa… wafanyakazi na vifaa vyao bila masharti,” Maphwanya amesema.
Hakuna vifaa vya SADC vitabaki. “SADC haiachi hata pini moja mashariki mwa DRC,” ameongeza.
Maafisa hawazungumzii ukubwa wa kikosi cha SAMIDRC, lakini idadi kubwa ya wanajeshi hao wanatoka Afrika Kusini, ambayo inasemekana kupeleka wanajeshi wasiopungua 1,300.
Wanajeshi wa Afrika Kusini pia wapo nchini DRC kama sehemu ya ujumbe tofauti wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani.
Wito wa waajeshi kuondoka nchini DRC umeongezeka nchini Afrika Kusini kufuatia vifo vya wanajeshi 14 wa Afrika Kusini katika eneo hilo mwezi Januari.
Wengi walikuwa sehemu ya ujumbe wa SADC, lakini angalau wawili walikuwa sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi watatu wa Malawi waliotumwa na SADC pia waliuawa, huku Tanzania ikisema wanajeshi wake wawili walifariki katika mapigano.
Kuondoka kwa wanajeshi wa SADC nchini DRC haikuwa ishara ya udhaifu au kutelekezwa kwa wale waliopatikana katika mapigano hayo, Maphwanya amesema.
“Kujiondoa kwetu ni hatua ya kiufundi ambayo inaruhusu kuendelea kwa amani na upatanishi.”
Kujiondoa kulikuja baada ya mshauri mkuu wa Rais wa Marekani Donald Trump barani Afrika kukutana na maafisa wa Kongo na Rwanda nchini Qatar wiki iliyopita, katika kile Marekani ilisema ni juhudi za kumaliza mgogoro huo.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na Marekani wanasema M23 imepata uungwaji mkono wa kijeshi kutoka kwa Rwanda, shutuma ambazo nchi hiyo imekanusha.