Afrika Kusini: Katu hatutaondoa kesi dhidi ya Israel ICJ licha ya vitisho vya Trump

Afrika Kusini imeapa kutoondoa kesi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), licha ya vitisho, mashinikizo na kukatiwa misaada na utawala wa Donald Trump.