
Nchini Afrika Kusini, mamia ya Waafrika Kusini walitoa heshima kwa Imamu Muhsin Hendricks siku ya Jumamosi, Machi 1, wakati wa maandamano ya Pride ya Cape Town. Imamu wa kwanza duniani mpenzi wa jinsia moja aliyejitokeza waziwazi, Hendricks aliuawa wiki mbili zilizopita. Jumuiya ya wapenzi wa jinsi moja (LGBTQIA+) inatumai uchunguzi wa uwazi na mwafaka kuhusu kile kinachoweza kuwa uhalifu wa chuki.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Joséphine Kloeckner
Mauaji ya Muhsin Hendricks yalikuwa kwenye mawazo ya watu wengi katika maandamano ya Pride ya Cape Town. Ilikuwa katika mji huu ambapo imamu, ambaye alijitokeza mnamo mwaka 1996, aliongoza wakfu na msikiti ulio wazi kwa Waislamu wote waliotengwa.
Uchunguzi wa uwazi na wa haraka
Wiki mbili baada ya mauaji yake yaliyotokea mchana ambayo yalishtua watu wengi duniani, bado hakuna mtu aliyekamatwa kwa kile ambacho wengi wanashuku kuwa uhalifu wa chuki. Rais Cyril Ramaphosa mwenyewe alizingatia uwezekano huu mwishoni mwa mwezi wa Februari na akaelezea wasiwasi wake. Polisi bado hawajathibitisha chochote.
Mashirika ya kutetea haki ya watu wa jamii ya wapenzi wa jinsia moja ( LGBTQIA+) yametoa wito wakufanyika kwa uchunguzi wa uwazi na wa haraka, jambo ambalo si mara zote wakati waathiriwa wanalengwa, mashirika hayo yameshutumu.
Afrika Kusini ndiyo nchi iliyoendelea zaidi katika bara hili linapokuja suala la uhuru wa mwelekeo wa kijinsia, na nchi pekee iliyohalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja, mwaka 2006. Hii haizuii ubaguzi na chuki zinazoendelea.