Afkham: Azimio la Bunge la Ulaya dhidi ya Iran halina msingi wa kisheria

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Haki za Binadamu na Masuala ya Wanawake ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema azimio lililopasishwa hivi karibuni na Bunge la Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu halina msingi wowote wa kisheria na linaonyesha tabia ya uingiliaji ya chombo hicho.