Afisa wa UN na Spika wa Bunge la Libya wajadili uchaguzi wa kitaifa na maridhiano

Stephanie Koury, naibu mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, jana Jumatatu alikutana na Spika wa Baraza la Wawakilishi lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo na walisisitizia umuhimu wa kuweko mchakato wa kina utakaowezesha kufanyika uchaguzi nchini humo.