Abuja yaijia juu Canada kwa kumyima ‘viza’ Mkuu wa Jeshi la Nigeria

Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Nigeria, Jenerali Christopher Musa, ameeleza kusikitishwa kwake na hatua ya ubalozi wa Canada katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, kumnyima yeye na maafisa wengine wakuu wa kijeshi viza ya kwenda Canada kuhudhuria hafla ya michezo ya maveterani wa vita huko Vancouver.