Abiria mmoja raia wa Uingereza aliyekuwa ameketi kiti namba 11A amenusurika katika ajali iliyohusisha ndege ya Air India aina ya Boeing 787-8 namba 171 mapema leo, Juni 12,2025.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 242 na ilikuwa ikitoka Mji wa Ahmedabad kuelekea Uwanja wa Ndege wa Gatwick nchini Uingereza, lakini ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ahmedabad. Uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea huku mamlaka zikihakikisha usalama wa manusura na kutoa huduma za dharura.
#azamnewsupdates
Mhariri|@official_jennifersumi