Abdul-Malik al-Houthi: Marekani ni mshirika wa jinai zote za Israel

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, Marekani ni mshirika wa jinai na uvamizi wote wa utawala haramu wa Israel.

Sayyid Abdul Malik al-Houthi amesema kuwa, adui Mzayuni anatumia njia ile ile nchini Lebanon aliyokuwa akiitumia huko Gaza na kuwalenga watu wote.

Amesema kuwa, tunachohitaji sisi kama Umma ni kuongeza hali ya kuwa macho na makini dhidi ya adui ili kuepusha hatari yake.

Kiongozi wa Ansarullah ameongeza kuwa: Jinai na ukatili wa Wazayuni vinatosha kuwafahamisha watu kuhusu dhati na utambulisho wa uvamizi wa utawala katili wa Israel.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ya Yemen amesema, Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinajaribu kufikia malengo yao ya pamoja katika uga wa kuwaangamiza Waarabu.

Aidha ameeleza kuwa, Marekani inajaribu kuuandalia mazingira utawala vamizi wa Israel ili uwe na mamlaka na satua ya kisiasa na kiuchumi katika eneo la Asia Magharibi.

Takribani Wapalestina 43,000 wameuawa shahidi tangu Oktoba mwaka jana wakati utawala haramu wa Israel ulipoanzisha hujuma na mashambulio ya kinyama dhidi ya Gaza

Kadhalika Seyyed Abdul Malik al-Houthi Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi ya Ansarullah ya Yemen amesema, Marekani na na madola ya Magharibi yanamsaidia adui Mzayuni kwa silaha na fedha na katika ngazi za kisiasa, na wakati huo huo zinajaribu kuficha jinai zinazofanywa kila leo na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na hivi sasa Lebanon pia.