Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi walijadili mambo gani?

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha kuhusu uungaji mkono ulioonyeshwa na nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa hatua ya maana iliyochukuliwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ya kukabiliana na mpango wa pamoja wa Marekani na utawala wa Kizayuni unaolenga kuifuta Palestina, na akabainisha kwamba: “Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuiunga mkono Palestina kwa msimamo thabiti.”