Gaza: Hamsini wauawa baada ya shambulio la Israeli karibu na kituo cha misaada

Kile ambacho kilipaswa kuwa usambazaji mwingine wa chakula na shirika la Gaza Humanitarian Foundation, linalosimamiwa na kufadhiliwa na Marekani na Israeli, kwa mara nyingine tena umegeuka kuwa mauaji.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Asubuhi ya Jumanne, Juni 17, huko Khan Yunis, watu wasiopungua 51 walmeuawa na mamia zaidi kujeruhiwa, kulingana na shirika la Ulinzi wa Raia wa Gaza. Mashahidi wa tukio halio wanasema kuwa jeshi la Israeli wamefanya mashambulizi kwa vifaru na ndege zisizo na rubani kwa raia waliokuja kuchukua chakula.

Tukio hilo limekuwa, kwa mara nyingine tena, la kutisha. Shahidi amerekodi video inayoonyesha miili ya Wapalestina iliyotapakaa ikiwa imetawanyika ardhini, mara tu baada ya mauaji hayo. “Wacha ulimwengu uone, ulimwengu wote uone, kuna makumi ya mashahidi, makumi ya mashahidi!” amelalamika shahidi huyo.

Raia hawa walikuwa wahasiriwa wa mashambulizi ya Israeli, kulingana na waandishi wa habari na mashahidi kwenye eneo la tukio, walipokuwa wakikusanya chakula kilichokuwa kinatolewa na na shirika la Gaza Humanitarian Foundation (GHF), linalosimamiwa na kufadhiliwa na Marekani na Israeli.

Takriban watu 50 wameuawa na 200 kujeruhiwa

“Baada ya dakika kumi tu ya usambazaji wa chakula, zoezi la kugawa chakula lilifunwa, na ndege zisizo na rubani na vifaru vimefanya mashambulizi dhidi ya raia waliokuwepo katika eneo hilo,” Eyad Amawi, mratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika Ukanda wa Gaza, amemwambia mwandishi wetu huko Jerusalem, Alice Moreno. GHF si chochote ila ni udanganyifu, chombo cha kuua, amesema. “Wanaweza kuruhusu Umoja wa Mataifa kushughulikia zoezi la kutoa misaada; wana ujuzi bora wa kazi hiyo. Shirika hili jpya la GHF ni udanganyifu mtupu kwa watu wetu, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kukomesha machafuko haya,” ameongeza Eyad Amawi.

Msemaji wa shirika la Ulinzi wa Raia wa Gaza Mahmoud Bassal ameliambia shirika la habari la AFP kuwa takriban watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa huku maelfu ya Wapalestina wakikusanyika asubuhi kupokea msaada huko Khan Younis.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika Hospitali ya Nasser

Wizara ya Afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas imeripoti kwamba baada ya masambulizi, “mashahidi 51 na watu zaidi ya 200 waliojeruhiwa” wamepelekwa katika hospitali ya Nasser huko Khan Younis, “watu 20 kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.” Siku moja kabla, shirika la Ulinzi wa Raia liliripoti watu 20 waliouawa katika shambulio la jeshi la Israeli walipokuwa wakitafuta msaada wa kibinadamu huko Rafah (kusini). Jeshi la Israeli kwa upande wake limehakikisha kuwa uchunguzi unaendelea.

Hospitali ya Nasser imezidiwa na watu wanatakiwa kupelekwa sehemu nyingine; Kwa hivyo timu za matabibu zinafanya kazi chini ya shinikizo na hofu ya shambulio jipya la Israeli.

Siku ya Jumatatu Juni 16, Wizara ya Afya ya Gaza ilitangaza kuwa watu 5,139 wameuawa tangu masambulizi ya Israeli kuanza tena Machi 18, baada ya kusitishwa kwa muda mfupi. Idadi ya vifo huko Gaza tangu kuanza kwa vita inafikia 55,432, kulingana na Wizara ya Afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *