Kenya na Tanzania zaongoza katika usambazaji wa dawa za kulevya: Ripoti

Ripoti ya kila mwaka tume ya kupambana na dawa za kulevya katika nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, inataja Kenya na Tanzania kuongoza katika usambazaji wa dawa hiyo kwenye ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kenya, Tanzania, Musumbiji na Afrika Kusini, yameorodheshwa kuwa kitovu cha usambazaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin kwenye masoko ya kimataifa  kutokana na uwepo wa bahari hindi ambalo hutumika kulagua mihidarati hiyo.

Waziri mambo ya ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen akisema hilo limetokana rushwa na utovu wa salama mipakani

‘‘Sharti nikiri kwamba hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la ulanguzi wa dawa kupitia Kenya na hili linasababisha vijana kutumia dawa hizo.’’ Alisema Waziri Kipchumba Murkomen.

Wajumbe katika mkutano kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya uliofanyika jijini Nairobi.
Wajumbe katika mkutano kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya uliofanyika jijini Nairobi. © @kipmurkomen

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Kgalema Motlanth ambaye pia ni mwenyekiti wa tume ya kupambana na mihadarati Kusini na Mashariki mwa Afrika, anasisitiza haja serikali za Afrika kuweka sera ya kuzuia usambazaji dawa za kulevya hasa Heroin na Cocain, ambazo vijana wengi Afrika wameanza kuzitumia, ripoti hiyo ikiashiria kwamba kufikia mwaka 2050 zaidi ya watu million 14 hapa Afrika watakuwa wanatumia mihadarati.

‘‘Tume imebaini kwamba uangalizi wa dawa za kulveya kwenye ukanda huu hauendani na sera za kutenda na kuzuia suala hilo.’’ Alisema Kgalema Motlanth

Matumizi ya mihadarati kadhalika yametajwa kuchangia kusambaa kwa magonjwa kama vile virusi vya ukimwi, ambayo kikandaa yamefikia asilimia 16.1.

Odrej Simek ni naibu mkuu wa tume ya Umoja wa Ulaya nchini Kenya.

‘‘Changamoto zinazotukabili zinaendelea kuwa ngumu zaidi na zinafanana kwa hivyo tunahitaji nguvu ya pamoja kuzingatia hilo.’’ Alisema Odrej Simek.

Viongozi hawa wamesema haya kwenye awamu 4 ya mkutano wa kupambana na mihadarati nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *