uuwanja wa Ndege wa Arusha ambao ulikuwa unatumika kwa safari za ndani tu, sasa utatumika kwa safari za nje ya nchi ili kurahisisha mkoa huo kufikika kirahisi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Arusha, Paul Makonda leo Juni 16, 2025 wakati akitembelea uwanja huo na kusema hiyo ni hatua kubwa itakayoondoa changamoto ya kupoteza muda mwingi barabarani hasa kwa wafanyabiashara pamoja na wageni wanaotoka nje ya nchi kwa shughuli za utalii.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa ndege Arusha, Edga Mwankuga ameahidi kuendelea kusimamia utoaji wa huduma bora kulingana na miongozo na taratibu ili kuwaridhisha wateja wao.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates