Watu kadhaa wauawa nchini Israel baada ya Iran kufanya mashambulizi mapya ya makombora

Usiku kucha, Israel na Iran zimeendelea na mashambulizi yao. Majeshi yote mawili yamewataka watu kukimbilia maeneo salama ili kujikinga na mashambulizi zaidi, huku idadi ya vifo vya raia katika pande zote mbili ikiongezeka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Israeli imefanya wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran siku ya Jumapili Juni 15 wakati Tehran nayo ikijibu kwa makombora mapya. Pande zote mbili zimetishia kufanya uharibifu zaidi katika mzozo ambao unaonekana kufukuta zaidi.

Iran imesema kuwa itaanza kufungua misikiti, vituo vya treni za metro na shule ili kutumika kama maeneo ya kujihifadhi, wakati Israel ikiendeleza mashambulizi. 

Nazo mamlaka za Israeli zimewaelekeza raia kuelekea kwenye maeneo salama ya kujikinga na mashambulizi.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa Mkuu wa ujasusi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi Mohammed Kazemi, ni miongoni mwa majenerali watatu waliuawa katika mashambuliziya Israel jana Jumapili.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amekataa mpango wa Israeli wa kumuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, Kulingana na BBC ikinukuu maafisa watatu wa Marekani ambao wameongea na mshirika wa BBC wa Marekani CBS News.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *