Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amemtaka Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuingiza bajeti ya Tuzo za Stadi za Ufundishaji zinzotolewa na Taasisi ya Elimu (TET) kwa walimu katika bajeti ya wizara hiyo ili tuzo hizo ziwe endelevu.
Profesa Mkenda ametoa agizo hilo Juni 14, 2025 mkoani Dar es Salaam wakati wa utoaji wa tuzo hizo kwenye hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Imeandaliwa na Esterbella Malisa
Mhariri @moseskwindi