Watu kadhaa wafariki kufuatia mvua kubwa nchini DRC na Congo-Brazzaville

Mvua kubwa iimenyesha na kusababisha mafuriko makubwa huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jumamosi, na kuua takriban watu 19, kulingana na mamlaka. Uharibifu pia umeripotiwa katika mji mkuu wa jirani, Brazzaville.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na wanahabari wetu huko Kinshasa na Brazzaville, Pascal Mulegwa na Loicïa Martial

Takriban watu 19 wamefariki dunia Jumamosi huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.

“Jioni ya leo, tuna vifo ya awali vya watu 19:kumi na saba katika wilaya ya Ngaliema (kaskazini-magharibi), wawili Lemba (katikati), na zaidi ya kaya 500 zimekumwa na mafuriko katika wilaya ya Matete (katikati),” amebainisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa katika ngazi ya kimkoa, Thierry Kabuya. Pia ameripoti “uharibifu mkubwa wa vifaa” na barabara “zimeharibiwa”.

Mvua hizi kubwa zinakuja wakati mji mkuu umekuwa katika msimu wa kiangazi kwa zaidi ya wiki mbili. Jambo la “ajabu”, kulingana na Augustin Tagisabo, mkuu wa kitengo cha mamlaka ya hali ya hewa huko Mettelsat, mamlaka ya Kongo inayohusika na utabiri wa hali ya hewa na satelaiti.

Hali hii adimu inatokana na mabadiliko ya tabianchi, hasa kutokana na “msimu wa kiangazi,” amesema. “Upepo wa kaskazini-magharibi kutoka Ghuba ya Guinea unaingia katika bara hilo kutoka magharibi. Unavuka Gabon, Kongo-Brazzaville, na jiji la Kinshasa, ukileta wingi wa mvua. Ni jambo la ajabu kwa kipindi hiki, na ni la muda,” mtaalamu huyo amesema.

Mamlaka ya tabianchi inafuatilia kwa karibu jambo hili “kwa sababu jinsi upepo unavyopenya zaidi, ndivyo hatari ya mvua kunyesha katika msimu wote inavyoongezeka,” amesema.

“Shambulio la ghafla”

Katika Brazzaville, mji mkuu wa Kongo, kimbuka hiki kikali kisichotarajiwa kimesababisha vifo vya watu watatu. Katika kitongoji cha Massengo, kaskazini mwa Brazzaville, barabara isiyo na lami inayounganisha parokia ya Saint-Grégoire na shirika la umma la nishati iko katika hali mbaya.

Haikuwa rahisi kuondoka nyumbani kwake ili kufika sehemu nyingine ya jiji. “Tulipotea katika kitongoji cha Mikalou, lakini kwa mafuriko, kama hapa, hatuwezi kuhama,” anasema kijana mmoja.

Mvua hiyo, katikati ya msimu wa kiangazi, imeshangaza wakazi wa Brazzaville, wengi wakiiona kuwa ni dhihirisho la mabadiliko ya hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *