Rais Samia Suluhu Hassan, amechangia shilingi milioni 100 kusaidia ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Kibah…

Rais Samia Suluhu Hassan, amechangia shilingi milioni 100 kusaidia ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Kibah…

Rais Samia Suluhu Hassan, amechangia shilingi milioni 100 kusaidia ujenzi wa uzio wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.

Akimuwakilisha Rais katika harambee hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mchango huo unaonyesha dhamira ya Rais ya kuhakikisha usalama wa wanafunzi. Harambee hiyo ilikusanya jumla ya shilingi milioni 510 kati ya milioni 700 zinazohitajika.

Majaliwa pia alihimiza halmashauri kutenga fedha za ndani kwa ujenzi na ukarabati wa shule. Mwenyekiti wa ujenzi, CPA Amos Makala, alisema lengo ni kuhakikisha watoto wa kike wanasoma katika mazingira salama.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *