Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema kuwa kwa siku inahitaji kati ya chupa 150 hadi 180 za damu ili kuwahudumia wagonjwa weny…

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema kuwa kwa siku inahitaji kati ya chupa 150 hadi 180 za damu ili kuwahudumia wagonjwa weny…

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imesema kuwa kwa siku inahitaji kati ya chupa 150 hadi 180 za damu ili kuwahudumia wagonjwa wenye uhitaji, lakini imekuwa ni changamoto kufikia kiwango hicho. Kwa sasa, hospitali hiyo hupata chupa takriban 50 pekee kwa siku, kiwango ambacho hakitoshelezi mahitaji ya kila siku.

Afisa Mhamasishaji wa Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Richard Masam amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililolenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa hiari.

Katika zoezi hilo, kampuni ya Jefag ilikuwa miongoni mwa taasisi zilizojitokeza na kuitikia wito huo, ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu kwa haraka.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *