Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga amelitaka shirika la TANESCO kuharakisha…

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga amelitaka shirika la TANESCO kuharakisha…

Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga amelitaka shirika la TANESCO kuharakisha upatikanaji wa vifaa ili miradi ya kimkakati ya ujenzi wa miundombinu ya umeme imalizwe kwa ufanisi na kwa wakati kuepusha ongezeko la gharama zitokanazo na ucheleweshaji wa miradi ili kupata matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Mhandisi Luoga ametoa maagizo hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya umeme ya gridi imara katika vituo vya umeme vya Ubungo I, Mabibo, Kinyerezi na Gongo la Mboto inayoendelea kujengwa kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

“Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa lakini vifaa vipatikane kwa wakati, wakandarasi waharakishe kazi na viwango vya kazi vizingatiwe” amesisitiza Mhandisi Luoga.

Miradi hiyo inalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme kwa kuboresha miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuongeza ubora wa huduma za umeme.

“Nimshukuru na kumpongeza Rais Samia kwa kuidhinisha rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii kwasababu uamuzi huo unaongeza tija kwa wananchi wa ndani na nje ya Dar es Salaam” ameongeza Luoga

Naye meneja wa miradi ya kuzalisha umeme kutoka TANESCO, mhandisi Abdallah Chikoyo ameahidi kuongeza usimamizi wa miradi na kuweka mipango kazi inayotekelezeka kwa wakati.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *