Ghana: Maafisa waandamizi 12 watuhumiwa kufuja dola Milioni za fedha za umma

Nchini Ghana, maafisa waandamizi kumi na mbili wa katika utawala wa rais wa zamani Nana Akufo-Addo wanatuhumiwa kwa wizi, utakatishaji fedha, matumizi mabaya ya ofisi ya umma kwa faida ya kibinafsi, na njama za uhalifu. Haya yamefichuliwa na Waziri wa Sheria siku ya Ijumaa, Juni 13. Uchunguzi wake ulikadiria ulaghai huo kuwa cedi milioni 548, sawa na dola milioni 53.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Accra, Victor Cariou

Ulaghai wa hali ya juu wa kifedha, uliofanywa kwa miaka sita mfululizo na maafisa wakuu wa Ghana. Orodha ya watuhumiwa iliyowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Michezo, Mustapha Ussif.

Yeye, pamoja na maafisa wengine kumi na moja, wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, ambazo awali zilikusudiwa washiriki wa huduma ya kitaifa. Mpango unaoajiri makumi ya maelfu ya wanafunzi kote nchini kila mwaka.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, washtakiwa hao wanadaiwa kuanzisha mfumo wa kuunda na kusajili washiriki feki katika utumishi wa taifa—na hivyo kuingiza bajeti iliyotengwa kwa njia isiyo halali.

Kuzidisha kwa pesa hizi kuliwezesha maafisa wakuu kuhusika kufuja zaidi ya cedi milioni 548 za fedha za umma, sawa na dola milioni 53. Hasara hizi zinaweza hata kukadiriwa katika mabilioni ya cedis, kulingana na chombo cha habari cha uchunguzi cha Ghana The Fourth Estate, ambacho ni chanzo cha ufichuzi huu.

Tangu kuchaguliwa tena kwa Rais John Dramani Mahama mwezi Januari, mamlaka inayotawala imeanzisha kesi kadhaa za kisheria dhidi ya maafisa wa utawala uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *