Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wanatarajia kunufaika na huduma ya uchunguzi wa saratani bure kwa muda wa siku nne, itakayofanyika ka…

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wanatarajia kunufaika na huduma ya uchunguzi wa saratani bure kwa muda wa siku nne, itakayofanyika ka…

Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wanatarajia kunufaika na huduma ya uchunguzi wa saratani bure kwa muda wa siku nne, itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni. Huduma hii imelenga kuwafikia wananchi wa kada zote ili kubaini mapema viashiria vya saratani na kuchukua hatua za matibabu kwa wakati.

Akizungumza wakati wa kutangaza huduma hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Diwani Msemo, amesema kuwa wataalamu mbalimbali wakiwemo madaktari bingwa watahudumu katika zoezi hilo. Dkt. Msemo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuanzia leo, Juni 14, ili kunufaika na huduma hizo muhimu.

#AzamTVUpdates
✍Jacob Ruvilo
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *