Wanandoa wameshauriwa kujenga utamaduni wa kushirikiana na kutegemeana kiuchumi ili kuimarisha mshikamano wa kifamilia na ustawi wa pamoja badala ya kila mmoja kujitegemea.
Mshauri na Mtaalamu wa Masuala ya Kifedha, Charles Ligonja amesema wanandoa wanapaswa kuweka malengo ya kifedha pamoja, kupanga bajeti ya familia kwa pamoja, na kupeana taarifa kuhusu hali ya kipato na matumizi. Alisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, wanandoa hujenga uaminifu, kuondoa migongano ya kifedha na kuimarisha mafanikio ya kifamilia kwa muda mrefu.
#AzamTVUpdates
✍Nifa Omary
Mhariri | John Mbalamwezi