
Boti kadhaa zilizama siku ya Jumatano joni Juni 11, kwenye Ziwa Tumba, lililoko kusini mwa Mkoa wa Equateur, kaskazini-magharibi mwa DRC. Ripoti ya awali inabainiha kuwa zaidi ya watu 40 waliangamia katika ajli hiyo, kulingana na mamlaka ya mkoa, na watu wengi wengine hawajulikani waliko. Shughuli za uokoaji bado zinaendelea.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi
Mitumbwi hiyo mitatu ilikuwa imekodiwa na familia moja ili kuuleta mwili wa mwanamke aliyefariki katika kituo cha afya cha Bikoro katika kijiji cha Ikoko Bongonda. Abiria wengine kisha walijiunga na msafara wa mazishi, kutia ndaniikiwa ni pamoja na watoto waliokuwa wakirejea nyumbani kwa likizo ya kiangazi. Hata hivyo, karibu saa 10 jioni, mawimbi makali na upepo mkali ulipindua boti hizo tatu, ambazo hazikuwa na koti za kuokoa maisha.
Watu waliofariki ni wengi. Takriban miili arobaini tayari imepatikana, kwa mujibu wa mamlaka ya mkoa, na takriban manusura thelathini wameokolewa, lakini wengi zaidi hawajulikani waliko. Kulingana na maelezo ya mashahidi, kati ya watu 100 na 200 walikuwa kwenye boti hizi, ambazo hazikuwa na orodha kamili za abiria kwa siku hiyo.
Wakati huo ho shughuli za kuwatafuta wahasiriwa zinaendelea. Baadhi ya abiria waliweza kukimbilia kwenye visiwa vidogo, kulingana na mjumbe wa timu ya uokoaji, ambaye ameongeza, hata hivyo, kwamba walikosa boti la kuwachukua.
Katika Bunge la taifa, Mbunge wa Equateur, Christophe Boulu, ametaja tukio hilo kuwa la kusikitisha na kutaka kuanzishwa kwa tume ya uchunguzi ya bunge. Mkoa huu mara kwa mara hukumbwa na maafa kutokana na ajali za boti. Mnamo mwezi Aprili, chini ya wiki, zaidi ya watu mia moja walifariki katika ajali mbili za boti zilizofuatana kwenye Mto Kongo.