Baadhi ya wananchi na wadau wa afya wameeleza matumaini yao kuhusu utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, wakisema sasa ndoto ya kila Mtanzania kupata huduma bora za afya iko karibu kutimia.
Wamepongeza hatua hiyo ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kwa kuanisha vyanzo mahsusi vya mapato vitakavyogharamia huduma hiyo kwenye #bajetikuu2025/26 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma.
Hata hivyo, wametoa wito kwa Serikali kuendelea kubuni vyanzo vya ziada vya mapato ili kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu, jumuishi na wa manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
#azamnewsupdates
Mhariri| @official_jennifersumi