
Jeshi la Israeli limefanya mashambulizi ya mabomu katika maeneo mengi nchini Iran usiku wa Alhamisi, Juni 12 kuamkia Ijumaa, Juni 13, yakiwemo maeneo ya nyuklia na viwanda vya makombora ya balistiki, na kuua makamanda wa kijeshi na wanasayansi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Israeli inaeleza kwamba imeanzisha Operesheni Rising Lion ili kuondoa “tishio” ambalo inaamini kuwa linatishia kuwepo kwake. Akitarajia jibu la Jamhuri ya Kiislamu, Waziri wa Ulinzi wa Israeli ametangaza hali ya hatari nchini humo.
Wimbi la mashambulizi ya anga kati ya Israel na Iran limeendelea kuibua hofu duniani, huku mashirika ya ndege yakibadili njia zao na masoko ya mafuta na hisa yakiyumba vibaya.
Iran ina mpango wake wa nyuklia inaosema kwamba ni kwa madhumuni ya amani. Irani inasisitiza kuwa haitafuti kutengeneza silaha za nyuklia, lakini nchi nyingi na shirika la kimataifa la kudhibiti nyuklia, Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), haziamini. Hata Israel pia haiamini kuhusu mpango huo.
Israel inauona mpango wa nyuklia wa Iran kama tishio la moja kwa moja kwa uhai wake. Kauli za viongozi wa Iran, hasa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, zimekuwa zikiihimiza kuharibiwa kwa Israel.
Licha ya kauli hizi mara nyingi kutafsiriwa kwa njia tofauti, huko Israel zinachukuliwa kwa uzito mkubwa, hasa kutokana na historia ya Wayahudi ya mauaji ya halaiki.
Mashambulizi ya Israeli kwenda Iran wiki hii imeongeza mvutano kati ya mataifa hayo, ukifikia kilele chake, huku msingi mkuu wa uhasama huu ukiwa ni mpango wa nyuklia wa Iran. Irani inasema “Israel itajuta ilichokifanya”.