Walinzi wa Mapinduzi waapa kulipiza kisasi kifo cha kiongozi wao

Walinzi wa Mapinduzi ya Iran wameapa kulipiza kisasi baada ya kifo cha kiongozi wao, Hossein Salami. Mashambulio haya “hayatabaki bila kujibiwa na (Israeli) lazima itarajie kulipizwa kisasi kikali na cha kusikitisha,” Walinzi wa Mapinduzi ya Kiisilamu wamesema katika taarifa iliyotolewa na runinga ya serikali.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran inasema ina “haki halali” ya kulipiza kisasi na inadai kuwa Marekani itawajibika kwa matokeo ya shambulio hilo.

Iran imeonya kuwa ina “haki ya kisheria na halali” ya kujibu mashambulizi mabaya yaliyotekelezwa na Israeli siku ya Ijumaa . “Kujibu uchokozi huu ni haki ya kisheria na halali ya Iran kwa mujibu wa Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa,” Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake na kuongeza kuwa jeshi la Iran “halitasika kulilinda taifa la Iran kwa nguvu zao zote.”

Iran pia imetangaza kuwa Marekani “itawajibika kwa matokeo” ya mashambulio ya Israeli. “Hatua za kichokozi za utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran hazingeweza kutekelezwa bila ya uratibu na idhini ya Marekani,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema, ikichukulia Marekani “kuwajibika kwa madhara hayo hatari.”

AIEA inathibitisha kwamba eneo la Natanz limelengwa

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (AIEA) limethibitisha leo Ijumaa kwamba eneo lenye utajiri la uran huko Natanz, katikati mwa Iran, limeathiriwa na shambulio la Israeli. “AIEA inafuatilia kwa karibu hali inayotia wasiwasi nchini Iran,” ameandika mkurugenzi wa shirika hiloRafael Grosi. “Shirika linaweza kudhibitisha kuwa eneo la Natanz ni moja wapo ya maeneo yaliyolengwa,” amesema, na kuongeza kuwa AIEA “inawasiliana na mamlaka ya Iran kuhusu viwango vya mionzi” na vile vile na wakaguzi wake kwenye eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *