Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum, amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kikao cha 27 cha mkutano wa 19 wa Baraza la Wawakilishi, kilichofanyika ukumbi wa baraza hilo.
Katika bajeti hiyo, Serikali imepanga kutumia kiasi cha shilingi trilioni 6.98, ikijumuisha mapato ya Serikali Kuu na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, imeelezwa kuwa uchumi wa Zanzibar unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.3 mwaka 2025, ukilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka 2024, huku idadi ya watalii ikitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 12.6 kutoka 736,755 hadi 829,929.
Ukuaji huo unatarajiwa kutokana na usimamizi madhubuti wa sera za kifedha, pamoja na upatikanaji wa nishati ya mafuta na gesi kwa gharama nafuu, hatua itakayosaidia kupunguza gharama za maisha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
#azamnewsupdates #bajetikuu2025
✍ Mtumwa Saidi
Mhariri | @official_jennifersumi