Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, amesema anatamani kuona bajeti ya mwaka huu ikijikita katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kupunguza mzigo kwa mwananchi wa kawaida.
Amesema kuwa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa kodi, hivyo kuna umuhimu wa serikali kuwa na mbinu mbadala za kuongeza mapato bila kuwaumiza wananchi.
Musukuma ametoa kauli hiyo katika kipindi maalum cha UTV kuelekea kusomwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali, akisisitiza kuwa ufanisi katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakamti, sambamba na ulinzi wa maslahi ya wananchi wa kawaida, kutasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo kwa haraka.
#AzamTVUpdates
✍Juliana James
Mhariri | John Mbalamwezi