Israel yawataka wakazi kuondoka baadhi ya maeneo ya Gaza

Katika tangazo lake, jeshi la Israel limewataka wakaazi kuondoka katika baadhi ya maeneo ya Gaza, likisema kuwa linafanya kazi ya kuwaangamiza magaidi na kuharibu miundombinu yake, huku likiwaelekeza watu kuhamia katika makazi yanayofahamika katika Ukanda huo kwa usalama wao.Wafanyakazi wa shirika la kiutu la GHF washambuliwa huko Gaza

Wakati tangazo hilo likitolewa, shirika la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa vikosi vya Israel vimefyatua risasi na kuwaua watu wasiopungua 13 na takribani 200 kujeruhiwa kwenyekituo cha kugawa chakula katika ujia wa Netzarim katikati mwa Gaza.

Vyanzo kutoka wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas, vimethibitisha tukio hilo vikitaja idadi ya waliouawa kuwa ni 10 na karibu 120 wamejeruhiwa. Katika taarifa nyingine shirika la WAFA limeripoti vifo vya watu watano waliouawa na vikosi vya Israel katika eneo la Sudaniya kaskazini magharibi mwa Gaza walipokuwa wakisubiri karibu na kituo cha kusambaza chakula.

Tizama namna Wapalestina wanavyopambania mkate

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Wanaharakati 8 kutimuliwa Israel na wengine wakamatwa Misri

Kwingineko, jumla ya wanaharakati wanane wanaounga mkono Palestina akiwemo mbunge wa Ufaransa katika Bunge la Ulaya wanatarajiwa kutimuliwa kutoka Israel, ikiwa ni siku tatu baada ya jeshi la wanamaji la Israel kuwazuia kusafiri kuelekea Gaza.

Wanaharakati wengine wanne kati ya 12 waliokuwamo katika boti ya misaada ikiwa ni pamoja na mwanaharakati wa Sweden Greta Thunberg, walikubali kuondoka Israel kwa hiari siku ya Jumanne, saa kadhaa baada ya boti yao kufikishwa mwambao.

Wanaharakati wanane waliokuwa wamesalia walikataa kuondoka wakiishutumu Israel kuchukua hatua zisizo halali na wamekuwa wakizuiliwa wakati mahakama ikipitia shauri hilo kisheria. Hata hivyo shirika la haki za binadamu la Israel la Adalah ambalo limetoa msaada wa kisheria, limesema kundi hilo limeshindwa kuzuia wanaharakati hao kurejeshwa kwao.

Gaza | Wapalestina
Wapalestina wakipita katikati ya mabaki ya nyumba zilizoharibiwaPicha: Jehad Alshrafi/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa nyingine inayohusiana na hilo, ni kwamba mamlaka za Misri zimewakamata zaidi ya wanaharakati 200 wanaounga mkono Palestina mjini Cairo kabla ya maandamano ya kimataifa kwa lengo la kuvunja mzingiro wa Israel dhidi ya Gaza.

Ikiwa ni sehemu ya maandamano ya kimataifa kuelekea Gaza, maelfu ya wanaharakati walipanga kusafiri hadi kwenye kivuko cha mpaka cha Misri cha Rafah kinachoingia ardhi ya Palestina siku ya Ijumaa ili kushinikiza kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu.

Msemaji wa maandamano hayo Saif Abukeshek alieleza kwamba wanaharakati waliokamatwa wanatoka mataifa tofauti ikiwemo Marekani, Morocco, Ufaransa na Algeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *