UN: Watoto bado wanatumika katika kazi hatarishi duniani

UN: Watoto bado wanatumika katika kazi hatarishi duniani

Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto, takwimu hizo mpya zinaonyesha kuwa angalau kiwango cha ajira kwa watoto kimepungua kwa watoto milioni 20 tangu mwaka 2020 ikilinganishwa na kati ya mwaka 2016 hadi 2020.

Licha ya maendeleo hayo, ulimwengu umeshindwa kufikia lengo lake la kutokomeza kabisa ajira kwa watoto kufikia mwaka huu wa 2025. Ripoti hiyo ya mwaka 2024, inatilia mkazo wa kwamba licha ya maendeleo hayo, mamilioni ya watoto bado wananyimwa haki ya kusoma, kucheza na kuwa watoto.

Mkurugenzi mtendaji wa ILO Gilbert F. Houngbo, amesema katika ripoti hiyo kwamba wazazi wenyewe wanapaswa kuungwa mkono na kuwezeshwa kupata kazi za maana ili waweze kuhakikisha kwamba watoto wao wapo madarasani na sio kuuza vitu sokoni au kwenye mashamba ili kuzisaidia familia zao.

Madagaskar 2022 |Mtoto akiwa katika kazi ya kuchimba madini
Madagascar-Mtoto akiwa katika kazi ya kuchimba madiniPicha: Safidy Andrianantenaina/UNICEF

Kwa mujibu wa takwimu, sekta ya kilimo ndio inayoongoza katika kuwatumikisha watotokwa asilimia karibu 61, ikifuatiwa na sekta ya utoaji huduma 27% kama vile kazi za majumbani na kuuza bidhaa sokoni huku sekta ya viwanda ikiwemo uchimbaji madini na uzalishaji ikichangia asilimia 13.

Kanda za Asia na Pasifiki zilishuhudia punguzo kubwa zaidi la ajira kwa watoto tangu mwaka 2020, huku kiwango cha ajira kwa watoto kikishuka kutoka asilimia 6 hadi asilimia 3.

Kanda ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara imebakia kubeba mzigo mkubwa, ikiwa na zaidi ya theluthi karibu mbili yaajira za watoto, sawa na watoto milioni 87. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 anasimulia sababu iliyomfanya kutafuta kibarua katika maeneo ya kuchimba migodi huko Sierra Leone..

“Jina langu ni Adama Sandy. Nina umri wa miaka 12, na ninafanya kazi kwenye machimbo huko Kenema. Familia yangu haina pesa ya kunipeleka shule kwa hiyo nawasaidia kufanya kazi ili kutafuta pesa ili wanipeleke shule. Asubuhi nafagia, ninaosha vyombo, nasafisha vyumba na kumfuata baba yangu, mama yangu kwenye machimbo ili kutafuta chochote. Nimekuwa nikifanya kazi kwenye machimbo haya kwa miaka mitano na siendi shule.”Ulinzi zaidi kwa watoto katika maeneo ya mizozo

Mtoto huyu anahadithia zaidi kuwa hana furaha pale anapowaona watoto wenzake wakiwa shule wakati yeye anakosa fursa hiyo. Anaziomba mamlaka zimwokoe atoke machimboni.

Matumaini kwa watoto waliokuwa wanajeshi

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

“Tunapovunja mawe watu huja kunyaunua, lakini hatuuzi zaidi ya 50,000 alfu kwa siku (kama dola 2) Pesa haitoshi kunipeleka shule; haitoshi kututengenezea chakula; haitoshi kututunza; haitoshi kutununulia nguo. Tunakula mara moja tu kwa siku, na kwa kawaida tunafanya hivyo jioni. Naomba mamlaka wanisaidie ili tuweze kuondoka kwenye machimbo haya na kurudi shule na kujifunza.”

Mashirika ya UNICEF na ILO yamezitaka serikali duniani kuwekeza katika ulinzi wa kijamii kwa kwa kaya zilizo katika mazingira magumu, kuimarisha mifumo ya ulinzi wa watoto na ufikiaji wa elimu bora kwa wote, hasa katika maeneo ya vijijini na yaliyoathiriwa na migogoro, ili kila mtoto aweze kujifunza, miongoni mwa mapendekezo mengi ili kutokomeza ajira kwa watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *