Walemavu wa macho wa Kata ya Mfinga, wilayani Sumbawanga, wamelalamikia vitendo vya uendeshaji mbovu wa pikipiki kutoka kwa baad…

Walemavu wa macho wa Kata ya Mfinga, wilayani Sumbawanga, wamelalamikia vitendo vya uendeshaji mbovu wa pikipiki kutoka kwa baad…

Walemavu wa macho wa Kata ya Mfinga, wilayani Sumbawanga, wamelalamikia vitendo vya uendeshaji mbovu wa pikipiki kutoka kwa baadhi ya madereva bodaboda ambao wamekuwa wakiwagonga na kuwahatarishia usalama wao.

Wamesema licha ya changamoto wanazopitia kila siku, bado wanakabiliwa na hofu ya ajali zinazotokana na kutokuzingatiwa kwa sheria za barabarani na ukosefu wa uelewa kwa baadhi ya waendesha bodaboda kuhusu haki na usalama wa watu wenye ulemavu.

Wameiomba Serikali na mamlaka za usalama barabarani kuchukua hatua madhubuti, ikiwemo kutoa elimu kwa madereva ili kuhakikisha usalama wao unazingatiwa.

#azamnewsupdates
✍️Sammy Kisika
Mhariri| @official_jennifersumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *