
Kutokana na kukwama kwa mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran, Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumatano, Juni 11, kwamba “haan imani” juu ya matokeo yake. Marekani itawahamisha wafanyakazi wasio wa lazima kutoka kwa ubalozi wake nchini Iraq.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hofu ya kuongezeka kwa hatari. Marekani imetangaza Jumatano, Juni 11, kupunguza wafanyakazi wa ubalozi wake nchini Iraq kwa sababu za kiusalama, huku Iran ikitishia kambi za Marekani katika Mashariki ya Kati iwapo kutatokea mzozo.
Iwapo mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yatafeli, ikiwa “migogoro itawekwa juu yetu, upande wa pili bila shaka utapata hasara zaidi kuliko sisi,” amesema Waziri wa Ulinzi wa Iran Aziz Nasirzadeh. “Kazi zao ziko ndani ya uwezo wetu,” na “Marekani italazimika kuondoka katika eneo hilo.”
“Kulingana na uchunguzi wetu wa hivi punde, tumeamua kupunguza idadi ya wanadiplomasia wetu nchini Iraq,” afisa wa Marekani ambaye hakutaka kutajwa jina lake amesema. Pia akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ametoa taarifa sawa na hiyo, akibainisha kwamba Rais Trump “amejitolea kuhakikisha usalama wa Wamarekani, ndani na nje ya nchi.” “Katika kuzingatia ahadi hii, tunatathmini mara kwa mara” viwango vya wafanyakazi katika balozi za Marekani, ameongeza.
Huko Baghdad, afisa mkuu wa usalama wa Iraq aethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba “wafanyakazi wasio wa lazima” wameondolewa kwenye ubalozi wa Marekani. “Tutajitahidi kuzuia shambulio lolote dhidi ya ubalozi,” afisa huyo, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema, akimaanisha “mawasiliano” na makundi yenye silaha yanayounga mkono Iran “ili kuwashawishi wasirushe risasi au kulenga” ujumbe wa kidiplomasia. Shirika la usalama wa baharini la UKMTO, linalosimamiwa na Jeshi la Wanamaji la Uingereza, limetoa maelezo mafupi ya onyo la “kuongezeka kwa mvutano” katika Mashariki ya Kati, hali ambayo inaweza kusababisha “kuongezeka kwa shughuli za kijeshi na athari ya moja kwa moja kwa wanamaji.”
Marekani ina kambi nyingi za kijeshi karibu na Iran, kubwa zaidi ikiwa nchini Qatar, ambako ndiko makao makuu ya Kamandi ya Mashariki ya Kati ya Jeshi la Marekani (CENTCOM).
Mkutano mpya usio na uhakika
Iran na Marekani, ambazo ziliwahi kuwa washirika wa karibu lakini zikizozana kwa miongo minne, zimekuwa na duru tano za mazungumzo ya nyuklia tangu mwezi Aprili, yaliyopatanishwa na Oman. Mazungumzo mapya yamepangwa kufanyika siku ya Jumapili, kulingana na Iran. Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa mkutano huo utafanyika siku ya Alhamisi, huku mpatanishi wa Oman hajazungumza lolote.