Karibia watu 50 wafariki katika mafuriko nchini Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini, watu karibu 50 wakiwemo wanafunzi wa Shule, wamepoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea  kwenye mkoa wa Cape Mashariki.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa mkoa huo, Oscar Mabuyane amesema hali inaendelea kuwa mbaya na kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya vifo kuongezeka.

Wanafunzi wanne wa shule na dereva wao ni miongoni mwa watu walipoteza maisha, baada ya basi lao kusombwa na maji ya mafuriko Jumanne asubuhi.

Mbali na maafa, mamia ya watu wameachwa bila makaazi, na kuwalazimu kujenga makaazi ya muda kipindi  hiki cha mvua kubwa.

Miongoni mwa waliofariki katika mafuriko hayo ni wanafunzi wa shule
Miongoni mwa waliofariki katika mafuriko hayo ni wanafunzi wa shule AP

Wizara ya elimu inasema shule 58 zimethiriwa, katika mkoa wa Cape Mashariki, huku zingine zaidi ya 60 katika wilaya tisa katika mkoa wa KwaZulu-Natal, zikiharibiwa.

Mbali na mafuriko, wakaazi wa mkoa huo pia kuanzia wiki hii, wanashuhudia baridi kali na upepo mkali na kuwaacha watu zaidi ya 500, bila umeme.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *