Wajumbe kutoka Kigali na Kinshasa kukutana tena wiki hii Marekani

Wajumbe kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Rwanda wanatarajiwa kukutana mjini Washington nchini Marekani tena wiki hii katika awamu nyingine ya mazungumzo yanayolenga kupata amani kati ya nchi hizo mbili.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maandishi yaliyoonewa na RFI yanaenda mbali zaidi kuliko tamko la kanuni lililosainiwa mwezi Aprili mjini Washington na mawaziri wa mambo ya nje wa Kongo na Rwanda.

Rasimu ya makubaliano ya amani ambayo inatarajiwa kutiwa saini Mjini Washngton inatoa masharti kwa Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake bila masharti katika ardhi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na hii ni pamoja na silaha na vifaa vilivyo pelekwa huko baada ya kuidhinishwa na serikali ya Kigali.

Waasi wa M23 huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 7 Aprili 2025.
Waasi wa M23 huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 7 Aprili 2025. REUTERS – Arlette Bashizi

Sharti la pili ni kuondolewa kwa hali ya dharura na kuzingirwa kwa mikowa ya Kivu kaskazini na Ituri iliyotangazwa tangu mwaka wa 2021. Hata hivyo makubaliano na Rwanda yanaweza tu kusainiwa baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya ana kwa ana mjini Doha Qatar kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23/AFC ambapo wanajadili pia juu ya suala la kusimamisha vita.

Mswada huo pia unazungumzia suala la waasi wa FDLR nchi hizo mbili zitaratibu kwa nia njema mpango wa kutambua, kutathmini, kutafuta njia za kuwatokomeza waasi hao wa FDLR.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *