
Wanaharakati wapatao 1,700 wameanza safari ya mabasi na magari kutokea mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wakiwemo 200 kutokea Algeria.
Wanaharakati hao wanatarajia kupitia Libya na Misri kufikia mpaka wa Rafah na Gaza kwa kile wanachosema ni kuwaunga mkono raia wa Gaza na kupinga vita vya Israel kwenye Ukanda huo.
Soma zaidi: Msafara wa wanaharakati wawasili Libya kuelekea Gaza
Chanzo kimoja cha usalama nchini Misri kimeliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba tayari zaidi ya wanaharakati 100 wametiwa nguvuni, wakiwemo 52 kutoka Ufaransa, 67 kutoka Algeria, 13 kutoka Moroko na wanane kutoka Libya.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Kantz, ameiomba Misri kuwazuwia wanaharakati hao kuingia Gaza, akidai kuwa kufanya hivyo kutahatarisha maisha ya wanajeshi wake, ambao kwa sasa wametwaa udhibiti wa Ukanda mzima ukiwemo mpaka wa Rafah.